Blogroll

ASANTE KWA KUTEMBELEA HABARI -24

Tuesday, May 3, 2016

TAARIFA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM

#KutokaDodoma Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi,  Mh Christopher Ole Sendeka amezungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Makao Makuu ya CCM , Dodoma.
Ndugu Sendeka anatoa taarifa kuhusu Kikao Cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika Ikulu ya Chamwino ambapo Kamati hiyo ilipitisha majina ya Wabunge 21 walioomba nafasi Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. Kikao hicho pia kimepitisha majina ya Viongozi walioomba kuziba nafasi zilizokuwa zimeachwa Wazi katika Wilaya na Matawi ya CCM nchini kote.

WHATSAPP YAZIMWA BRAZIL KWA SAA 72

Hakimu mmoja nchini Brazili amefunga mawasiliano ya mtandano wa simu kwa njia ya whatsapp kwa saa 72.

Hakimu huyo Marcel Montalvao amesema kampuni inayomiliki mtandao huo imeshindwa kusaidia kutoa taarifa katika kesi ya uhalifu.

Mwezi Machi, Montalvao aliamuru kukamatwa kwa afisa mwandamizi wa Facebook katika nchi za Kilatini bwana Diego Dzoran baada ya kukataa kutoa ushirikiano katika uchunguzi dhidi ya dawa za kulevya.

Wamiliki wa mtandao huo wa Whatsapp ambao pia wanamiliki mtandao wa Facebook wamesema kuwa wamekatishwa tamaa na kitendo hicho kwa kuwa wamekuwa wakitoa ushirikiano wa kutosha mahakamani.

Mtandao huo umekuwa ukifungiwa mara kadhaa nchini Brazil kwa miezi michache ya karibuni kwa sababu zinazofanana na hizo.
==========

A regional judge on Monday ordered all telephone operators in Brazil to block WhatsApp, the popular messaging app owned by Facebook, for failing to turn over data as part of an ongoing drug trafficking investigation.

Starting about 2 p.m., the app ceased to function, a move sure to frustrate and anger Brazilians who use the messaging and free-calling functions regularly.

According to the Sergipe state tribunal's website, the app will be blocked for 72 hours.

Jan Koum, CEO and co-founder of the messaging service, posted a statement on his Facebook page in response to the blocking:
"Yet again millions of innocent Brazilians are being punished because a court wants WhatsApp to turn over information we repeatedly said we don't have," it said. "Not only do we encrypt messages end-to-end on WhatsApp to keep people's information safe and secure, we also don't keep your chat history on our servers. When you send an end-to-end encrypted message, no one else can read it -- not even us."

This is not the first time WhatsApp has been targeted by judges. In March, the vice president of Facebook Latin America was detained after authorities said Facebook refused to release data from WhatsApp in the interest of protecting its users.

Last December, a Sao Paulo state judge blocked the service for 48 hours after WhatsApp failed to respond to two court orders "in a criminal investigation."

Facebook has not commented.

Source: CNN

Friday, April 29, 2016

WATUMISHI HEWA KINONDONI

HABARI YA BOSS WA TIC

#KuperuziNaKudadisi - TanzaniaDaima
JK amponza bosi wa TIC
●Atumbuliwa kwa kitochukua mshahara wa miaka mitatu
●Padri Kassala ateuliwa kuwa Askofu Geita
UKAWA wamgombea  Ndugai
●Waapa kutoshiriki chaguzi za Kamati.
●Zomeazomea yaibuka bungeni
●Rufaa ya kina Zombe leo.

JPM AMTIMUA MWINGINE

JPM NA JESHI LA POLICE

#HabariClouds Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi nchini na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujirekebisha kwa kutekeleza wajibu wao huku wakitanguliza maslahi ya taifa.
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo wakati akifungua kikao cha kazi cha Makamanda wa polisi wa mikoa, Mawakili wafawidhi wa serikali wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi, kinachofanyika kwa siku mbili Mjini Dodoma.

Aidha, Rais Magufuli ameitaka Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujipanga kufanya kazi kwa ufanisi na ameelezea kusikitishwa na vitendo vya serikali kushindwa katika kesi nyingi mahakamani licha ya kuwa na wanasheria mahiri.

Hata hivyo Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi na ofisi ya Mkurugenzi wa  Mashitaka kwa kazi kubwa wanayoifanya na ametaka apelekewe mpango wa mahitaji yao ili atafute namna ya kuimarisha vyombo hivyo.

MMAREKANI AHUKUMIWA KIFUNGO NA KAZI NGUMU KOREA


Raia wa Marekani amefungwa jela miaka 10 na kazi ngumu nchini Korea Kaskazini baada ya kupatikana na makosa ya kufanya ujasusi, shirika la habari la Uchina la Xinhua limeripoti.
Kim Dong-chul, raia wa Marekani aliyezaliwa Korea Kusini, alikamatwa mwezi Oktoba mwaka jana.
Kim aliwasilishwa kwa wanahabari mjini Pyongyang mwezi jana na akaoneshwa akikiri makosa, na kusema kwamba alilipwa na Korea Kusini kufanya ujasusi.
Mwezi Machi, mwanafunzi mwingine Mmarekani alifungwa jela miaka 15 kwa kujaribu kuiba bango la propaganda.
Alipatikana na makosa ya "uhalifu dhidi ya dola”.
Kim amefungwa jela katika kipindi ambacho uhusiano baina ya Korea Kaskazini na Umoja wa Mataifa, Marekani na nchi nyingine za Magharibi umedorora.
Majuzi, Pyongyang imefanya msururu wa majaribio ya kurusha makombora baada ya kufanyia majaribio bomu ya nyuklia mwezi Januari, majaribio yote yakivunja vikwazo zilivyowekwa na UN.
Pyongyang ilijaribu kurusha makombora mawili ya masafa ya wastani Alhamisi lakini yalilipuka na kuanguka baharini muda mfupi baada ya kurushwa.
Hatua hiyo ilipelekea kuitishwa kwa mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Source Efm radio

Thursday, April 28, 2016

MARK CLATTENBURG REFEREE OF MAN U v/s CRYSTAL PALACE

Mark Clattenburg will referee the FA Cup final between Manchester United and Crystal Palace at Wembley Stadium on May 21.It will be the first FA Cup final Clattenburg has officiated and he will be assisted by John Brooks, Andrew Halliday and fourth official Neil Swarbrick. Clattenburg, a Premier League referee since 2004, said:

"It came out of the blue. These days you get told of what games you're doing by text, but when you see a call coming in from the FA referees' department you know it's important.

DC HAPI ATEMBELEA WANANCHI BUNJU, MBWENI LEO.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh. Ally Hapi leo amewatembelea wananchi maeneo ya Bunju na Mbweni waliokuwa na kero mbalimbali.
Katika eneo la Bunju Kilungule, baadhi ya wananchi nyumba zao zimezungukwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Mkuu wa Wilaya akiambatana na Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es salaam na mainjinia wa manispaa alitembelea eneo hilo na kuona adha inayowapata wananchi.
Akipokea maelezo ya Mwenyekiti wa serikali ya mtaa na baadae kuzungumza na wananchi wa eneo hilo, mkuu wa wilaya aliambiwa na baadhi ya wakazi wa asili wa eneo hilo kuwa sehemu hiyo ilikua ni bwawa la maji miaka yote.
Wakazi hao ambao nyumba zao zimezungukwa na maji walimuomba Mkuu wa wilaya kusaidiwa pampu kubwa ili maji hayo yavutwe na kupelekwa kwenye mitaro upande wa pili wa barabara.

Akijibu maombi hayo Mh. Hapi aliwaagiza mainjinia wa manispaa kuhakikisha kuwa wanafanya utaratibu wa kupata pampu kubwa ya kuvuta maji hayo. Aidha, Mkuu huyo wa wilaya ya Kinondoni aliwaambia wananchi kuwa wale wote waliojenga  katika eneo hilo ambalo ramani inaonesha kuwa ni eneo la wazi wajiandae kuondoka.

"Serikali itawasaidia kutoa haya maji kama hatua ya dharura. Lakini suluhu ya kudumu ni kuwa waliojenga hapa wote wamejenga eneo la wazi tena ni bwawa. Hivyo lazima wajiandae kuhama.
Serikali kazi yake ni kuwaambia wananchi ukweli, hata kama ukweli huo utakua na maumivu. Hivyo ukweli wa jambo hili ni kuwa waliojenga hapa wahame."

Akitoa rai kwa viongozi wa serikali ya mtaa ambao wameshiriki katika kuuza eneo hilo kinyume na taratibu mh. Mkuu wa Wilaya aliagiza na kusema

" kila Mwananchi aliyejenga hapa aende ofisi ya mtaa kujisajili akiwa na vielelezo vyote vya kumiliki eneo hili na alikonunua. Kisha nipewe taarifa na uhakiki utafanyika. Kama kuna viongozi wa serikali ya mtaa walishiriki kuuzia watu viwanja hapa kinyume na ramani ambayo wao wana nakala yao basi wajiandae kuwajibishwa."

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya alitembelea eneo la Mbweni ambako Mwananchi asiyefahamika amejenga ukuta kuzunguka eneo la wazi. Hapi alifika eneo hilo na kujionea ukuta huo kisha akaagiza mtendaji wa mtaa pamoja na anayejenga ukuta huo kufika ofisini kwake kesho Ijumaa mchana wakiwa na vielelezo vyote na vibali vya ujenzi kama wanavyo.

Ziara ya mkuu wa wilaya inaendelea muda huu katika maeneo ya barabara za Sinza ambazo wakandarasi walipewa kujenga.

Monday, April 25, 2016

DC HAPI ATEMBELEA UPANUZI WA BARABARA YA MWENGE-MOROCCO LEO.


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Salum Hapi leo ametembelea ujenzi unaoendelea wa upanuzi wa barabara ya Mwenge-Morocco kuona maendeleo yake. Barabara hiyo ambayo ilikua na kero kubwa ya foleni iliamriwa kupanuliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli katika hatua yake ya kubana matumizi na kupeleka fedha katika shughuli za maendeleo.
Katika ziara yake hiyo Mh. Hapi alitembea umbali wa mita 500 kwa miguu kukagua pia usafi wa mazingira ya kando ya barabara ambapo alipofika katila kituo cha mafuta cha Total, aliagiza uongozi wa kituo kufanya usafi wa mazingira yaliyo mbele ya kituo chao.
Aidha Mh. Mkuu wa Wilaya pia alizungumza na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam, Mkandarasi na wataalam wengine wa ujenzi na kujua maendeleo yao.
Meneja wa TANROADS na Mkandarasi walimueleza Mkuu wa wilaya kuwa tayari kazi imekamilika kwa asilimia 90 na kwa mbali wanatarajia kukabidhi mwezi June mwaka huu.

LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK

TUFWATILIE INSTAGRAM