Blogroll

ASANTE KWA KUTEMBELEA HABARI -24

Friday, April 22, 2016

MEYA WA KINONDONI AMFAGILIA DC WA KINONDONI KWENYE KIKAO

MEYA WA KINONDONI AMFAGILIA DC HAPI KIKAONI
Meya wa manispaa ya Kinondoni Mh. Boniphace leo amemuelezea Mkuu wa wilaya ya Kinondoni kuwa ni mtu mwenye historia ya uchapakazi, msimamo usioyumba na mwenye uwezo mkubwa wa kusimamia uadilifu. Meya ameyasema hayo akifungua kikao cha baraza la madiwani wa manispaa ya Kinondoni ambapo alimualika Mh. Mkuu wa Wilaya Ally Salum Hapi kusalimia na kutoa salamu zake kwa baraza hilo. Mheshimiwa Meya Boniphace ameliambia baraza hilo kuwa anamfahamu Mh. Hapi kwakua amesoma nae chuo Kikuu cha Dar es salaam alipokua anasoma masomo ya ualimu.
"Nilimfahamu pale Chuo Kikuu alipokua anasomea Sheria nami ualimu, japo yeye alikua reli ya Kati (CCM) nami nilikua reli ya Tazara (Chadema) tangu wakati huo hadi sasa. Ninamuamini katika uwezo wake na kasi ya uchapakazi. Hakika Rais Magufuli hajakosea kukuteua."

Katika hatua nyingine Meya amemuahidi Mkuu wa Wilaya Hapi ushirikiano wote katika kupambana na changamoto za wananchi wa Kinondoni za madawati, watumishi hewa, ardhi na ufisadi.
Katika salamu zake baada ya kukaribishwa, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Hapi alimshukuru Mstahiki Meya kwa heshima kubwa aliyompa na kumuahidi kuwa ataiongoza vema Kinondoni katika kutatua kero za wananchi. Hapi alieleza kuwa vipaumbele alivyovitoa Mh. Rais vya watumishi hewa, madawati, afya , usafi na vita dhidi ya rushwa ndiyo mambo ambayo tayari ameanza nayo.
"Siamini kama Kinondoni inaweza kuwa na watumishi hewa 34 pekee. Nimeagiza kazi zaidi ifanyike, na kikao idara ya manispaa ifungue mafaili mapya la uhakiki yenye picha ya kila mtumishi, barua yake ya ajira na nyaraka zote zinazoonesha majukumu yake na aliko. Hii ni katika kubaini nani ni nani, yuko wapi na anafanya nini wakati wa ukaguzi wa ana kwa ana."
Mkuu huyo wa wilaya ya Kinondoni amesema tayari watumishi hewa wasiopungua 10 wamekamatwa na wengine 7 wamelipa fedha kiasi cha milioni 40 walizotia hasara serikali.
"Mchana wa leo nimetaka taarifa ya maandishi kutoka kwa Ofisi ya Mkurugenzi juu ya watumishi hewa. Ndani ya saa 1 nikapewa taarifa kuwa tayari hiyo na kuagiza vyombo vya dola viwakamate watumishi hewa waliobakia."
Kuhusu msimamo wake juu ya Kinondoni Mkuu wa Wilaya alisema kuwa Rais amemuamini na kumtuma kuwatumikia wana Kinondoni, na kwamba atafanya kazi hiyo usiku na mchana.
"Nimetangaza vita dhidi ya rushwa, maana Kinondoni inanuka rushwa. Watumishi wote wasio waadilifu wanaoiba pesa za umma na kujinufaisha wao na familia zao nitashughulika nao.
Aidha watumishi wanaomiliki makampuni na kujipa tenda kwa mlango wa nyuma wajiandae, maana nitawasaka popote walipo na sheria itachukua mkondo wake. Hapi alisema sheria na taratibu za utumishi wa umma haziruhusu mtumishi wa umma anayetoa huduma kutangaza tenda ofisini kwake na kisha kuipa kampuni yake au ya familia take.
Akitoa shukrani kwa niaba ya baraza, Mbunge wa Ubungo Saidi Kubenea amemshukuru Mh Mkuu wa Wilaya na kuahidi kumuunga mkono katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi.
Hata hivyo Mh. Kubenea ametaka sheria na taratibu kufuatwa ili kuhakikisha hakuna mtu anayeonewa katika mapambano hayo.
Baraza la madiwani la Manispaa ya Kinondoni lilikutana leo saa 11 jioni katika ukumbi wa manispaa.

No comments:

Post a Comment

LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK

TUFWATILIE INSTAGRAM